Bohari ya Dawa-MSD, imesema kiwango cha ununuzi wa dawa kutoka kwa wazalishaji kimeongezeka kutoka asilimia 18 kwa robo ya kwanza ya mwaka 2024/2025 kwa wazalishaji wa ndani na nje na kufikia asilimia 57 kwenye robo ya nne ya mwaka.
Ununuzi huo umefanyika kwa lengo la kuwa na uhakika wa upatikanaji wa bidhaa za afya na kuwezesha MSD kupata bei ambayo ni nzuri.
Mfamasia kutoka Kitengo cha Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa MSD, Bwiro Magesa, amesema MSD inaendelea na jitihada za kuwalinda na kuwawezesha wazalishaji wa ndani na hadi sasa wazalishaji wanazalisha aina 238 za dawa na sabuni za kutakasa mikono kupitia viwanda 12.
Aidha, thamani ya ununuzi imeendelea kuongezeka na kufikia zaidi ya shilingi Bilioni-98 kwa mwaka wa fedha 2024/2025, kutoka shilingi Bilioni-15.9 kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Hata hivyo, katika kipindi cha mwezi Julai 2025 hadi Februari mwaka 2026, bidhaa za afya zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni-66.3 zimenunuliwa kutoka kwa wazalishaji wa ndani.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni