Breaking


Jumatano, 22 Aprili 2026

EWURA YAHAMASISHA UJENZI WA VITUO VIJIJINI.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), April 21, 2026, imetumia fursa ya Wiki ya Nishati kuwahamasisha waheshimiwa wabunge kuwekeza katika ujenzi wa vituo vya mafuta maeneo ya vijijini pamoja na vituo vya CNG ili kuendelea kusogeza huduma kwa wananchi.

Kaimu Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Wilfred Mwakalosi, amesema kuwa EWURA inatumia maonesho hayo kutoa elimu kuhusu namna inavyohakikisha upatikanaji wa huduma za nishati na maji kwa wakati na kwa gharama nafuu.

Amebainisha kuwa wabunge ni wawakilishi wa wananchi, hivyo kuwajengea uelewa kuhusu udhibiti, fursa za uwekezaji na utaratibu wa kupokea na kushughulikia migogoro na malalamiko kutawawezesha kuwasilisha taarifa sahihi kwa wananchi kuhusu juhudi za Serikali katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za umeme, mafuta na gesi asilia.

Akizungumza katika maonesho hayo, Ofisa Mwandamizi wa Kitengo cha Mafuta, Mhandisi. Ibrahim Kajugusi, amesema elimu inayotolewa pia inalenga kuwafahamisha wananchi jinsi EWURA inavyosimamia upatikanaji wa huduma za mafuta nchini kwa kuzingatia ubora uliopitishwa na gharama sahihi.

Hakuna maoni: