Breaking


Jumatano, 22 Aprili 2026

MKUTANO KUHUSU MLANGO-BAHARI WA HORMUZ KUFANYIKA LONDON

Wataalam wa kijeshi kutoka nchi zaidi ya 30 watakutana leo mjini London katika mkutano utakaojadili namna ya kuhakikisha ulinzi katika Mlango-Bahari wa Hormuz mara tu vita vya Iran vitakapomalizika.

Mkutano huo utakaoongozwa na Uingereza na Ufaransa, unalenga kuandaa mikakati madhubuti wa kulinda meli za mafuta, kama walivyojadili wiki iliyopita mjini Paris, Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron.

Mazungumzo hayo yatakayofanyika Northwood Kaskazini mwa jiji la London yatazingatia uwezo wa kijeshi, masuala ya amri na udhibiti, kutegua mabomu ya ardhini na jinsi vikosi vya kijeshi vinavyoweza kupelekwa katika eneo hilo la Mlango-Habari wa Hormuz.

Hakuna maoni: