Iran na Marekani zimetoleana kauli za vitisho zikitumishiana Misuli wakati haijafahamika wazi ikiwa duru ya pili ya mazungumzo ya amani, huko Islamabad itafanyika.
Pakistan inaendelea na maandalizi ya mkutano huo, huku taarifa zikieleza kuwa Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance, atasafiri leo kuelekea Islamabad kuhudhuria mazungumzo hayo ikiwa yatafanyika.
Rais wa Marekani, Donald Trump, ametishia kuishambulia vikali Iran ikiwa haitafikia makubaliano mapya, huku Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Khalibaf, akitaja kuwa wamejiandaa vilivyo na wako tayari kuonesha mbinu mpya kwenye uwanja wa vita.
Hayo yanajiri wakati makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda wa wiki mbili yaliyoanza kutekelezwa Aprili 8, yanatarajiwa kufikia tamati leo usiku, hali inayozusha hofu ya kuzuka tena kwa vita hivyo vya Mashariki ya Kati.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni