Breaking


Alhamisi, 9 Aprili 2026

JKCI KUTOA HUDUMA YA UPANDIKIZAJI MOYO NCHINI


Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete-JKCI, imeanzisha mchakato wa kutoa huduma za upandikizaji wa Moyo, hatua inayolenga kuboresha huduma za matibabu ya magonjwa ya Moyo na kuiweka Tanzania katika ramani ya huduma za kibingwa duniani.

Akizungumza leo jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dokta Peter Kisenge, amesema taasisi hiyo ilifanya upembuzi yakinifu mwaka 2025 na kuunda kamati maalum iliyoweka dira ya utekelezaji wa huduma hiyo.

Kamati hiyo imekamilisha kazi na kukabidhi rasimu ya muongozo wa uanzishwaji wa huduma za upandikizaji wa Moyo mwezi Januari, huku hatua inayofuata ikiwa ni kuwapeleka wataalamu wa JKCI katika hospitali kubwa duniani kwa ajili ya mafunzo na kujifunza uzoefu wa huduma hizo.

Lengo la JKCI ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 inakuwa miongoni mwa hospitali zinazotoa huduma ya upandikizaji wa Moyo duniani.

Hakuna maoni: