Breaking


Jumatatu, 20 Aprili 2026

LATRICIA LAN ATWAA TAJI LA MISS WORLD TANZANIA 2026

Mashindano ya Miss World Tanzania 2026 yamehitimishwa kwa kishindo huku mrembo Latricia Lan akitangazwa mshindi na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika jukwaa la kimataifa la Miss World. 


Akiwakilisha Dar es Salaam, Latricia ameonyesha mchanganyiko wa urembo na akili kupitia mradi wake wa “Nuru ya Elimu” unaolenga kuwawezesha vijana kielimu na kijamii. 

Katika ushindani huo mkali, Nouru Masoud ameibuka mshindi wa pili (1st Runner-Up), akifuatiwa na Paulina Allute (2nd Runner-Up), huku Silya Mussa na Dian Rutagalinda wakishika nafasi za tatu na nne mtawalia, matokeo yanayoakisi ushindani mkubwa na vipaji vya hali ya juu mwaka huu.


Hakuna maoni: