Polisi wa Israel wanasema maeneo matakatifu ya Yerusalemu yatafunguliwa tena kwa wageni na waumini kufuatia mpango wa muda wa kusitisha mapigano uliofikiwa katika mzozo wa Mashariki ya Kati.
Maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na eneo la msikiti wa Al-Aqsa, Ukuta wa Magharibi unaojulikana kama Western Wall, na Kanisa la Kaburi Takatifu, yote yakiwa kwenye Jiji la Kale, ni miongoni mwa maeneo matakatifu zaidi duniani katika Uislamu, Uyahudi na Ukristo.
Kwa sababu ya vita dhidi ya Iran vilivyoanzishwa na Marekani na Israeli wiki sita zilizopita, maeneo hayo yamefungwa wakati wa sikukuu muhimu za kidini, ikiwa ni pamoja na wakati wa Pasaka huku idadi ndogo sana ya makasisi ikikubaliwa.
Jiji la Kale, ambapo maeneo yake kwa kawaida huwa na shughuli nyingi za wakazi, wanaoenda sokoni, watalii na waumini, limekuwa kimya sana, huku wamiliki wengi wa maduka na vibanda wakishindwa kufungua kabisa.
Polisi walisema kwamba maeneo matakatifu yatafunguliwa tena kuanzia Alhamisi asubuhi, huku mamia ya maafisa wengine wakipelekwa ili kuhakikisha usalama, na umma unahimizwa kuwa na subira ikiwa kutakuwa na msongamano.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni