Wakati rapa Offset akiendelea kupona baada ya tukio la kutisha la kupigwa risasi katika Seminole Hard Rock Hotel & Casino, bado maisha yake yanaonekana kuwa kwenye misukosuko mikubwa safari hii si ya afya tu, bali pia ya kifedha.
Habari zinadai kuwa Offset anakabiliwa na deni la takribani dola 100,000 (zaidi ya milioni 265 za Kitanzania) alilokopa kutoka MotorCity Casino Hotel, ambapo alipewa mkopo huo ili kuendeleza “starehe za usiku” za kamari mnamo Machi 2024.
Kwa mujibu wa nyaraka zilizoripotiwa na TMZ, juhudi za kasino hiyo kumtafuta Offset zilikwama, na hata walipojaribu kujichukulia fedha moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yake kama walivyokuwa wamekubaliana inaelezwa kuwa hakukuwa na salio la kutosha kulipia deni hilo.
Hali hii imezua mjadala mkubwa mitandaoni, huku mashabiki wakijiuliza kama staa huyo wa zamani wa kundi la Migos anaingia kwenye kipindi kigumu zaidi cha maisha yake.
Kana kwamba hiyo haitoshi, kati ya mwaka 2025 hadi mapema 2026, Offset amekuwa katikati ya mgogoro mzito wa talaka na rapa Cardi B. Inasemekana Offset anadai kupata msaada wa kifedha kutoka kwa Cardi B, akisisitiza kuwa mchango wake ulikuwa mkubwa katika kujenga chapa yao ya pamoja.
Wakati huo huo, rapa Lil Tjay naye ameibuka na madai mapya, akidai Offset anamdai dola 10,000 alizomkopesha kwa ajili ya kamari baada ya kuishiwa pesa.Pamoja na drama hizi zote risasi, madeni, na migogoro ya kimahusiano swali kubwa linabaki: Je, hii ni dalili ya kuporomoka kwa Offset, au ni moja ya vipindi vya changamoto ambavyo mastaa hupitia kabla ya kurejea kwa nguvu zaidi? Muda utaamua, lakini kwa sasa, maisha ya Offset yanaendelea kuwa kama filamu ya kusisimua isiyo na mwisho.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni