Breaking


Jumapili, 26 Aprili 2026

MHE. LUSWETULA ASHIRIKI UZINDUZI MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula, ameshiriki katika Hafla ya Uzinduzi wa Meli ya Kwanza ya Uvuvi wa Bahari Kuu, iliyofanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), Kigamboni, Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Aprili, 2026.

Katika Uzinduzi huo Mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na imehudhuriwa na viongozi Mbalimbali wa Serikali wakiwemo Mawaziri na Naibu Mawaziri kutoka Wizara mbalimbali, , Waheshimiwa Wabunge, Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali.




Serikali inatarajia kuongeza meli nyingine nne ikiwa ni juhudi zinazolenga kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kukuza uchumi wa nchi uliokusudiwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050. Aidha, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuialika Sekta binafsi kutumia fursa za kushiriki katika miradi na shughuli mbalimbali za kukuza uchumi wa nchi na maisha ya wananchi.

Hakuna maoni: