Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV, ameanza awamu ya nne na ya mwisho ya safari yake barani Afrika kwa kuitembelea Guinea ya Ikweta ambako alipokelewa na umati mkubwa katika nchi hiyo yenye Wakatoliki wengi.
Akiwa mjini Malabo, Papa Leo amelaani kile alichokiita "ukoloni wa kuyapora madini ya Afrika" na "tamaa ya madaraka", kauli aliyoitoa katika nchi inayoongozwa na Rais Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, mwenye umri wa 83 na aliye madarakani tangu mwaka 1979.
Hata hivyo, Papa Leo, amepangiwa baadaye kuzungumza na Rais Nguema, viongozi wa serikali, wanadiplomasia pamoja na wawakilishi wa asasi za kiraia na pia ataongoza misa kubwa katika uwanja wa Malabo kabla ya kukamilisha safari yake ya siku 10 katika nchi nne za Afrika.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni