Malkia wa muziki Rihanna hatimaye amewaonyesha mashabiki wake sura ya binti yake Rocki Irish Mayers kwa mara ya kwanza kupitia jarida la W Magazine, na mtandao mzima umechafuka kwa furaha. Mtoto huyo mwenye umri wa mwaka mmoja tayari ameanza kuandika historia kwa kusainiwa kama “mtoto wa gharama kubwa zaidi Hollywood” kwenye cover hiyo, akivunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na North West. Ni kama alivyozaliwa na nyota kichwani.
Wengi hawaachi kuzungumzia mvuto wa mtoto huyo, wakijiuliza kama amefanana zaidi na mama yake Rihanna au baba yake, A$AP Rocky. Mitandaoni, mashabiki wamegawanyika wapo wanaosema ni copy-paste ya mama, huku wengine wakiona sura ya baba imetawala. Lakini jambo moja liko wazi, huyu si mtoto wa kawaida bali “nepo baby” anayekuja kwa kasi ya radi kwenye ulimwengu wa umaarufu.
Kwa sasa, macho yote yako kwa Rocki, ambaye tayari ameanza safari ya staa kabla hata hajajua kutamka jina lake vizuri. Kama mwanzo ndio huu, basi mashabiki wanajiandaa kuona mtoto huyu akikua akiwa icon mpya wa kizazi kijacho. Swali linabaki palepale kwako wewe, anafanana zaidi na nani?

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni