Breaking


Jumanne, 21 Aprili 2026

KISIMA B5 KITALU CHA MNAZI BAY CHAZALISHA GESI ASILIA MARA MBILI ZAIDI YA MATARAJIO.

Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishwaji Wazawa na Wadau kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA),  Charles Nyangi, amesema uwezo wa kuzalisha gesi katika kisima B5 katika kitalu cha Mnazi Bay mkoani Mtwara umekuwa zaidi ya mara mbili ya ilivyotarajiwa.

Hatua hiyo inatoa taswira ya Tanzania kuwa miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa gesi asilia.

Nyangi ametoa kauli hiyo Aprili 21, 2026, wakati wa akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi Asilia katika maonesho ya Wiki ya Nishati inayoendelea katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Amesema takwimu za kisima B5, ambacho tayari kimekamilika, zimeonyesha uzalishaji uko juu ya matarajio ya awali.

“Tumekamilisha uchimbaji wa kisima kimoja kule Mnazi Bay. Matarajio yalikuwa tupate futi za ujazo milioni 20, lakini kisima kinatoa futi za ujazo milioni 45. Kwa hakika, tupo mahali pazuri zaidi.”Amesema.Nyangi

Nyangi amesema kwa sasa PURA inaendelea na uchimbaji wa kisima cha pili, ambapo hadi leo asubuhi uchimbaji umefikia mita 1,500, huku utafutaji zaidi ukiendelea na kukiwa na matumaini ya kupata gesi nyingi zaidi.

Pia amesema Serikali, kwa kushirikiana na wadau, inaendelea kuwekeza zaidi katika utafutaji na uchimbaji wa gesi, na mwelekeo ni mzuri kwa siku za usoni ili nishati hiyo izidi kuwanufaisha Watanzania.

Hakuna maoni: