Breaking


Jumanne, 21 Aprili 2026

KAMPUNI YA DP WORLD YAWEKEZA ZAIDI ZAIDI YA DOLA MIL -125

   

Kampuni ya DP World iliyowekeza katika Bandari ya Dar es salaam iwekeza kiasi cha dola za kimarekani Milioni -125 katika kipindi cha miaka miwili sawa na 96% tangu kuanza kazi April 07 mwaka 2023. 

Katika kipindi cha miaka mitano Kampuni ya DP World iliahidi kuwekeza Dola za Kimarekani Milioni 250 katika uwekezaji wa miundombinu katika Bandari ya Dar es salaam. 

Akizungumza na Wahariri wa vyombo vya Habari katika bandari ya Dar es salaam Meneja Uhusiano wa Kampuni ya DP World Elitunu Mallamia amesema katika kipindi cha miaka miwili ya utendaji kazi kumekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo ongezeko la utoaji wa mizigo kulinganisha na kipindi cha miaka iliyopita. 

Ametolea mfano wa mwaka 2023 walifanikiwa kutoa jumla ya kontena 165,545 ambapo kwa mwaka 2025 walifanikiwa kutoa jumla ya kontena 323,837 ongezeko la asilimia 96. 

Mallamia amesema katika Robo ya mwaka huu 2026 tayari wamehudumia zaidi ya Kontena Laki Moja na 10 huku wakitarajia kuhudumia Tani Milioni 30 za mizigo kufikia mwishoni mwa mwaka huu 

Amesema uwekezaji wa vifaa na miundombinu ndani ya bandari imechangia kwa kiasi kikubwa kutoa mizigo kwa haraka ambapo kwa sasa meli ya mizigo inakaa kati ya siku 7 mpaka 11 kushusha mzigo bandarini. 

Meneja Uhusiano huyo wa Kampuni ya DP World amesema tayari wameboresha na wanaendelea kuboresha mifumo na matumizi ya TEHAMA ili kuendelea kufanyakazi kwa uwazi zaidi ambapo kwa sasa kumekuwa na muingiliano kati ya Kampuni ya Dp World na Mamlaka ya Mapato Tanzania

Hakuna maoni: