Wanafunzi wa shule ya sekondari Faraja Seminary wametembelea Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kilimanjaro kwa lengo la kujifunza masuala ya kodi na faida zake katika maendeleo ya taifa.
Ziara hiyo ya mafunzo imefanyika April 24,2026 ambayo imelenga kuwajengea wanafunzi hao uelewa mpana kuhusu wajibu wao kama walipakodi wa baadae nchini.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Afisa mwezeshaji biashara kutoka TRA, Bw. Salehe Mayange amesema utoaji wa elimu ya kodi kwa wanafunzi ni kujenga jamii yenye misingi ya uwajibikaji katika taifa.
Aidha, Katika mafunzo hayo wanafunzi walipata fursa ya kupata elimu ya athari za magendo kwa jamii, Faida za ulipaji wa kodi pamoja na kodi zitokanazo na ushuru wa bidhaa na forodha.
Kwa upande wake Mwalimu aliyeambatana na wanafunzi hao Bw. Riziki Yowezel ameishukuru TRA na kusema kua elimu hiyo walioipata kwa vitendo itawapa uelewa mpana zaidi na kua mabalozi wazuri wa kodi kwa baadae.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni