Ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya mafunzo kwa timu kutoka Uganda ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii, Wanyamapori na Malikale wa nchi hiyo, Doreen Katusiime ya kupata uzoefu wa namna Tanzania ilivyofanikiwa katika utekelezaji wa miradi ya kupambana na ujangili na biashara haramu ya nyara
Timu hiyo ipo nchini Tanzania na alhamisi tarehe 23, Aprili 2026 imetembelea Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kupata maelezo juu ya mradi wa kupambana na ujangili na biashara haramu ya nyara kwa kutumia njia jumuishi, wa Serengeti North mradi unaotekelezwa chini ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro ikiwa ni miongoni mwa programu zinazofanyika chini ya mradi wa kupambana na ujangili na biashara haramu ya nyara (IWT Project).
Ujumbe huo kutoka Uganda upepata nafasi pia ya kutembelea vivutio na kufanya mafunzo katika eneo la hifadhi la Ngorongoro na katika eneo la Makumbusho la Jiopaki ya Ngorongoro-Lengai
Huu ni mpango maalumu wa ziara za mafunzo baina ya nchi zinazotekeleza Miradi yenye malengo yanayoshabihiana ili kubailishana uzoefu na kujifunza namna nchi nyingine inavyotekeleza Mradi wake.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni