Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametoa wito wa kuanza tena kwa mazungumzo kati ya Marekani na Iran, akieleza matumaini kuwa hatua hiyo itasaidia kumaliza vita.
Alisisitiza kuwa ni “dhahiri kabisa kwamba hakuna suluhisho la kijeshi kwa vita hii.
António Guterres pia alisema ana wasiwasi mkubwa kuhusu "ukiukwaji wa wazi wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu" huko Gaza.
Guterres pia alisema kuwa usitishaji mapigano “lazima udumishwe kikamilifu” na kwamba “ukiukwaji wote lazima ukome,” akiongeza: “Natoa wito wa kurejea kwa mazungumzo ili kufikia makubaliano.”
Aidha, Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alizitaka nchi zote “kuheshimu uhuru wa usafiri wa majini, ikiwemo katika Mlango wa Hormuz, kwa mujibu wa sheria za kimataifa.”

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni