Breaking


Jumanne, 14 Aprili 2026

PAPA LEO XIV ATOA WITO WA MSAMAHA NCHINI ALGERIA

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV amewasili mjini Algiers, Algeria, kwa ziara ya kihistoria katika nchi hiyo yenye Waislamu wengi na akatoa wito wa msamaha kwa waathiriwa wa vita vya uhuru nchini humo.

Akitoa hotuba ya heshima kwa waathiriwa wa vita vya uhuru wa nchi hiyo kutoka kwa Ufaransa vya mwaka 1954-1962, Papa Leo alitoa wito wa "msamaha.

''Mahali hapa tukumbuke kuwa Mwenyezi Mungu anataka amani kwa kila taifa, amani ambayo si ya kukosekana kwa migogoro tu, bali ya kielelezo cha haki na utu.  Amani hii ambayo inatuwezesha kuangazia siku zijazo kwa roho ya upatanisho, inawezekana tu kupitia msamaha.''

Muda mfupi kabla ya kuondoka Roma, Papa Leo mzaliwa wa Marekani alikosolewa hadharani na Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alikashifu matamshi ya Papa Leo ya kutaka kusitishwa kwa vita nchini Iran.

Hakuna maoni: