Breaking


Jumamosi, 18 Aprili 2026

WAZIRI MKUU NCHEMBA AAGIZA WAFANYAKAZI UWANJA WA ARUSHA KULIPWA KWA WAKATI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amemtaka Mkandarasi  wa Uwanja wa Arusha na Wasimamizi wa uwanja huo kuhakikisha kila mtu anayefanya kazi katika uwanja huo analipwa kwa wakati.

Ametoa agizo hilo Aprili 17, 2026 wakati alipofanya ziara kwenye uwanja huo, akisistiza kuwa, mkandarasi atakayekiuka atafungiwa kufanya kazi Tanzania.



Amesema ameridhishwa sana na maendeleo ya ujenzi huo, akiongeza kuwa, hiyo ni hatua kubwa ya uwekezaji uliofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya michezo nchini.

Hakuna maoni: