Breaking


Jumamosi, 18 Aprili 2026

RAIS SAMIA ATAZINDUA MELI YA UVUVI WA BAHARI KUU APRILI 25, 2026 - DKT BASHIRU



Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani anatarajiwa kuzindua Meli ya Kwanza ya Uvuvi wa Bahari Kuu , ambapo uzinduzi wake utafanyika Makao Makuu ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO ) Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amesema hayo Aprili 17, 2026, wakati wa ziara ya  Kamati ya Uchumi na Uwekezaji ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kutembelea na kukagua ujenzi wa bahari ya uvuvi Kilwa Masoko Mkoani Lind na kuieleza kamati hiyo kuwa  bandari ya uvuvi Kilwa masoko iliyogharimu shilingi bilioni 280 baada ya kukamilika itafanyiwa majaribio kabla ya kukabidhiwa kwa serikali.

“ Mradi huu kwa sawa  tuko asilimia 97, asilimia tatu zilizobaki ni kwa sababu kuna mitambo mingine imeagizwa ili ifungwe halafu tufanye majaribio kabla ya kukabidhiwa, wakati wowote ndani ya mwezi wa nne na watano mkandarasi anaweza kutukabidhi” alisema Mhe. Balozi Dkt. Bashiru.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Uwekezaji ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Makame Mohammed Sufiani amepongeza maono ya Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Mwinyi kwa kujana na maono ya ujenzi wa bandari ya uvuvi itakayochochea ukuaji wa sekta ya uvuvi na uchumi wa buluu.

Naye Naibu Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe. Mboja Ramadhan Mshenga amesema baada ya kujifunza kuhusu  ujenzi wa bandari ya uvuvi eneo la Kilwa Masoko na Zanzibar pia itajenga bandari ya uvuvi ili kukuza uchumi wa buluu.

Ziara hiyo pia imehudhuriwa na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara , Kilimo na Uvuvi (KKB -VBKM) Mhe. Livingstone Lusinde aliyeambatana na Wajumbe wawili wa Kamati hiyo.

Hakuna maoni: