Breaking


Ijumaa, 10 Aprili 2026

WAZIRI NDEJEMBI AKUTANA NA KAMPUNI ZA EQUINOR NA SHELL KUJADILI UTEKELEZAJI WA MRADI WA LNG NCHINI.

Waziri wa Nishati,Deogratius Ndejembi amekutana na kufanya mazungumzo na Kampuni ya Equinor Tanzania AS pamoja na Shell Exploration and Production Tanzania Ltd kuhusu utekelezaji wa uchimbaji wa gesi ya LNG katika mikoa ya kusini.

Katika kikao hicho kilichofanyika April 10,2026,Jijini Dar es salaam, Waziri Ndejembi amekutana na viongozi wa makampuni hayo, akiwemo Menno Bax, Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Shell Exploration and Production Tanzania Ltd, pamoja na Hilde Merete Nafstad, Makamu wa Rais na Meneja wa Nchi wa Utafutaji na Uzalishaji wa Kimataifa (EPI) wa Equinor Tanzania AS.

Mazungumzo hayo pia yamewashirikisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio, na Kamishna wa Mafuta na Gesi kutoka Wizara ya Nishati, Goodluck Shirima.



Makampuni hayo yanajihusisha na utafiti, uchimbaji na uendelezaji wa gesi asilia baharini, pamoja na kushiriki katika maandalizi na utekelezaji wa mradi wa gesi iliyoyeyushwa (LNG) nchini Tanzania

Hakuna maoni: