Breaking


Jumanne, 12 Mei 2026

“𝐑𝐈𝐒𝐊 𝐂𝐇𝐀𝐌𝐏𝐈𝐎𝐍𝐒” 𝐖𝐀 𝐏𝐃𝐏𝐂 𝐖𝐀𝐏𝐀𝐓𝐈𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐘𝐀 𝐔𝐒𝐈𝐌𝐀𝐌𝐈𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐕𝐈𝐇𝐀𝐓𝐀𝐑𝐈𝐒𝐇𝐈


Waratibu na wasimamizi wa vihatarishi (Risk Champions) wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), leo tarehe 12 Mei, 2026 katika ukumbi wa chuo cha VETA uliopo Jijini Dodoma wamepatiwa mafunzo ya usimamizi wa vihatarishi ili kuongeza uelewa wa kutambua, kuchambua na kudhibiti vihatarishi vinavyoweza kuathiri utendaji kazi wa shughuli za PDPC na Serikali kwa ujumla.

Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa PDPC, Dkt. Emmanuel Mkilia, katika kufungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Tafiti za Ulinzi wa Taarifa na Teknolojia - PDPC, Dkt. Noe Nnko amewataka maafisa hao kufuatilia kwa makini mafunzo hayo ili kuboresha uwajibikaji katika eneo la kazi.



Mafunzo hayo yanatolewa na Afisa Ukaguzi Mkuu kutoka Wizara ya Fedha Bi. Adolphina Lugendo na yatafanyika kwa siku nne kuanzia leo mpaka tarehe 15 Mei, 2026.

 


Hakuna maoni: