Crawford ambaye ni mmoja wa mabondia waliotamba duniani kwa rekodi ya kutopoteza pambano katika michezo yake ya kulipwa, alitoa kauli hiyo alipokutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa ziara yake nchini Tanzania.
Katika mazungumzo hayo, bondia huyo alieleza kuwa ana hamu kubwa ya kushuhudia vivutio maarufu vya utalii nchini ikiwemo Hifadhi ya Taifa Serengeti, Ngorongoro Conservation Area pamoja na Zanzibar ambavyo ni miongoni mwa maeneo yanayovutia watalii kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Kwa upande wake, Dkt. Abbasi alimkaribisha rasmi nchini kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, na kumpongeza kwa mchango wake mkubwa katika mchezo wa ndondi duniani.
Aidha, alimweleza kuwa Tanzania itaendelea kuwa mahali salama na rafiki kwa wageni pamoja na watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani, huku akimkaribisha kuendelea kutembelea nchi hiyo wakati wowote atakapopata nafasi baada ya kutangaza kustaafu mchezo wa ndondi mwishoni mwa mwaka 2025.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni