Breaking


Jumanne, 26 Mei 2026

DAVIDO AKAMILISHA AHADI YA KULIPIA MAZISHI YA ALEXX EKUBO


Msanii maarufu wa muziki wa Afrobeats, Davido, ameripotiwa kukamilisha ahadi yake ya kugharamia mazishi ya aliyekuwa mwigizaji wa filamu za Nollywood, Alexx Ekubo.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali za burudani nchini Nigeria, Davido alitoa ahadi hiyo kwa familia ya marehemu ikiwa ni sehemu ya kuonyesha upendo, mshikamano na kuthamini urafiki waliokuwa nao kwa muda mrefu. Hatua hiyo imeelezwa kugusa wengi, huku mashabiki wakimsifu msanii huyo kwa kuendelea kuwa karibu na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu.

Alexx Ekubo alifariki dunia Mei 11, 2026 akiwa na umri wa miaka 40, baada ya kuripotiwa kusumbuliwa na saratani ya figo kwa muda. Taarifa zinaeleza kuwa alifariki akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Evercare, iliyopo mjini Lagos.

Familia ya marehemu imetangaza kuwa mazishi yake yanatarajiwa kufanyika Juni 18, 2026 katika kijiji cha Ujari, eneo la Arochukwu, jimbo la Abia State.

Kifo cha Alexx Ekubo kimeacha simanzi kubwa katika tasnia ya filamu ya Nollywood, ambapo alikuwa mmoja wa waigizaji waliopata umaarufu mkubwa kupitia filamu mbalimbali zilizovutia watazamaji barani Afrika.



Hakuna maoni: