Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, ameongoza kikao maalum cha kupitia mapendekezo ya mpango wa kuzalisha umeme kwa kutumia teknolojia ya nyuklia ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuongeza uzalishaji wa umeme nchini na kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa maendeleo ya Taifa.
Katika kikao hicho imeelezwa kuwa tayari hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa ikiwemo kuandaa rasimu ya mpango wa nyuklia pamoja na kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomi (IAEA).
Mpango huo unatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka sita hadi saba kupitia awamu mbalimbali zitakazohusisha utayari wa nchi, maandalizi ya sheria na ujenzi wa miundombinu ya kuzalisha umeme kwa kutumia teknolojia ya nyuklia.
Kikao hicho kimefanyikaMei 16, 2026 katika Ofisi Ndogo za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anaheshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, Mtendaji Mkuu wa TANESCO, Lazaro Twange pamoja na wataalamu wengine kutoka wizarani.



.jpeg)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni