Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeendelea kuongeza kasi ya utoaji wa hati za ardhi huku ikiwaonya wamiliki wa viwanja na mashamba wanaoshindwa kuendeleza maeneo yao kwa mujibu wa sheria za umiliki.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi Dkt.Leornad Akwilapo akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2026/2027,Mei 28 bungeni Jijini Dodoma amesema katika mwaka 2025/2026 ilipanga kuandaa na kusajili hatimiliki 500,000, hati za hakimiliki ya kimila 520,000, hati za sehemu ya jengo 1,000, vyeti vya ardhi ya kijiji 100 pamoja na kusajili miamala ya hatimiliki na nyaraka za kisheria 100,000.
Amesema hadi Mei 15, 2026, Wizara ilikuwa imeandaa na kusajili hatimiliki 107,683 sawa na asilimia 21.54 ya lengo, huku hati za hakimiliki ya kimila zilizotolewa zikifikia 99,762 sawa na asilimia 19.19 ya lengo.
Aidha, vyeti vya ardhi ya kijiji vilivyotolewa vilifikia 148 sawa na asilimia 148 ya lengo, wakati hati za sehemu ya jengo zilizotolewa zilifikia 914 sawa na asilimia 91.4 ya lengo.
Kutokana na mafanikio hayo, Wizara imepanga katika mwaka 2026/2027 kuandaa na kusajili hatimiliki 200,000, hati za hakimiliki ya kimila 300,000, vyeti vya ardhi ya kijiji 60, hati za sehemu ya jengo 1,000 pamoja na miamala ya hatimiliki na nyaraka za kisheria 100,000.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni