Ugonjwa huo unaendelea kuwa chanzo kikubwa cha vifo vinavyotokana na magonjwa yasiyoambukiza duniani kutokana na wengi kutogundulika mapema au kutopata matibabu sahihi kwa wakati.
Kwa mujibu wa WHO, bara la Afrika linaongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha watu wenye shinikizo la damu ambapo takribani asilimia 44 ya watu wenye umri wa miaka 30 hadi 79 wanaathirika.
Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa ongezeko hilo linachangiwa na ulaji usiofaa, matumizi makubwa ya chumvi, kutofanya mazoezi, unywaji wa pombe pamoja na uvutaji wa sigara.
Nchini Tanzania, ugonjwa wa shinikizo la damu umeendelea kuwa changamoto kubwa ya afya ya jamii huku tafiti zikionesha kuwa watu wengi wanaishi na ugonjwa huo bila kufahamu hali zao.
Wataalamu wa afya wanaonya kuwa mabadiliko ya mtindo wa maisha pamoja na msongo wa mawazo vinaongeza idadi ya wagonjwa hasa mijini.
Makundi yaliyo katika hatari zaidi ni pamoja na watu wenye uzito mkubwa, wenye historia ya ugonjwa huo katika familia, wenye kisukari, watumiaji wa tumbaku na pombe pamoja na watu wanaokosa kufanya mazoezi mara kwa mara.
Aidha, wataalamu wanasema vijana nao wameanza kuathirika zaidi kutokana na mfumo wa maisha wa kisasa usiozingatia afya.
Madaktari wanashauri wananchi kupima presha mara kwa mara, kula lishe bora yenye matunda na mboga za majani, kupunguza matumizi ya chumvi pamoja na kufanya mazoezi ili kupunguza hatari ya kupata shinikizo la juu la damu ambalo limeendelea kuitwa “silent killer” kutokana na kutokuwa na dalili za wazi kwa baadhi ya wagonjwa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni