The Weeknd ambaye kwa sasa ni mmoja wa wasanii wanaosikilizwa zaidi duniani, aliulizwa iwapo idadi kubwa ya wasikilizaji wake wa kila mwezi kwenye Spotify inamfanya kuwa mkubwa kuliko aliyekuwa akijulikana kama “Mfalme wa Pop”, Michael Jackson.
Akijibu swali hilo, msanii huyo alisema wazi kuwa hakuna anayefikia kiwango cha Michael Jackson katika historia ya muziki.
“Usiwahi kunilinganisha na THE GOAT. Namba za Spotify hazimaanishi kuwa umefikia kiwango cha Michael Jackson katika enzi yake. Hakuna mtu aliye hai anayemgusa Michael Jackson, hata mimi,” alisema The Weeknd.
Kauli hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa muziki duniani, huku wengi wakimsifu The Weeknd kwa heshima yake kwa historia na mchango mkubwa wa Michael Jackson kwenye tasnia ya muziki wa kimataifa.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni