Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron ametangaza uekezaji mpya barani Afrika wakati mkutano wa kilele wa ushirikiano ulipofika Nairobi, nchini Kenya.
Rais Macron amesema Ufaransa itawekeza dola bilioni 27 katika sekta tofauti barani Afrika ikiwemo nishati, Akili Unde-AI na kilimo.
Rais huyo, amesema zaidi ya dola bilioni kumi na sita zitatoka kwenye kampuni za Ufaransa na dola bilioni 10.5 kutoka Afrika.
Rais wa Kenya Wiliam Ruto, katika hotuba yake alisisitiza suala la uhuru wa mataifa ya Afrika akitaja neno 'uhuru' mara 8 katika hotuba hiyo.
Mkusanyiko huo wa viongozi wa Afrika mjini Nairobi umefanyika wakati ambapo mahusiano ya Ufaransa na makoloni yake ya zamani hasa mataifa ya Afrika Magharibi yakiwa yamevurugika.
Ufaransa kwa muda mrefu imekuwa ikitumia sera ya baada ya ukoloni ya udhibiti wa kiuchumi, kisiasa na kijeshi iliyopewa jina 'Francafrique' ikiwemo kuweka maelfu ya vikosi vyake vya jeshi katika mataifa ya Afrika ambayo ilikuwa inayadhibiti.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni