Ule usemi wa Samaki mkunje angali mbichi, unatakiwa kufanyiwa kazi na Wazazi, walezi nchini, kuzungumza na vijana wao juu ya mambo yanayochangia upatikana wa mimba za Utotoni.
Hii ni kutokana na Wazazi wengi kutokuwa na utamaduni wa kuzungumza ukweli na Watoto wao juu ya upatikanaji wa mimba za Utotoni kwa vijana Balehe, ambao wengi wanakosa kupata taarifa sahihi kwa wazazi wao na kupokea taarifa zisizo sahihi nje hali inayochangia wengi kupata mimba za utotoni.
Akizungumza katika sehemu za mada katika mafunzo ya waandishi na watangazaji wa habari wanaofanya vipindi vya watoto, malezi na maadili, Mwezeshaji wa Kitaifa kuhusu masuala ya vijana balehe na Mimba za Utoto na VVU, Madgalena Dinawi, amesema Wazazi wanatakiwa kubadilika ili kusaidia watoto kupata taarifa sahihi kutoka kwao.
Amesema njia ya Mzazi Kuzungumza na vijana balehe, wa Kike na Kiume kwa uwazi kwa kumueleza hatua na mabadiliko ya mwili wake kutamsaidia mtoto kupata taarifa sahihi.
Amebainisha kuwa zipo sababu zinazochangia vijana kupata mimba, ikiwepo kukosekana kwa taarifa sahihi ya elimu kuhusu afya ya uzaz na jinsia, Mmomonyoko wa maadili, malezi na makuzi katika Jamii, kuiga tabia ya kunywa pombe na matumizi ya dawa za kulevya, msukumo wa makundi rika, na kubakwa.
Ameeleza kuwa ili kusaidia Jamii kupunguza changamoto hiyo, Vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuandaa vipindi na maudhui ya kuibadilisha jamii, kuwaeleimisha wazazi na walezi umuhimu wa kuzungumza na watoto wao kwa uwazi kwani ufichaji wa taarifa na aibu zimechangia mtoto kukosa taarifa sahihi.
Kwa upande wao baadhi ya Waandishi na watangazaji wanaoshiriki mafunzo hayo wamesema ipo haja ya kuibeba
dhana ya familia bora, ijengwe kupitia misingi ya kitamaduni ya malezi ya watoto kwa kuzingatia vipengele muhimu ikiwemo Kumjali, Kumlinda na Kuzungumza nae, kuwa agenda katika vipindi vyao.
Mafunzo hayo yanayoratibiwa kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia wanawake, na makundi Maalum, na kufadhiriwa na shirika la Kimataifa linalohusika na kulinda haki, kuboresha afya, elimu na ustawi wa watoto na wanawake duniani ( Unicef) yamewakutanisha zaidi ya waandishi 40 kutoka upande wa Radio, magazeti, televisioni, na blog ili kuhakikisha jamii inafikiwa na kuleta mabadiliko chanya.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni