Breaking


Ijumaa, 8 Mei 2026

MSHTUKO INSTAGRAM! RONALDO, MESSI, SELENA NA KARDASHIANS WAPOTEZA MAMILIONI YA FOLLOWERS KWA MASAA 24


Mastaa wakubwa duniani wamejikuta kwenye headline baada ya kupoteza mamilioni ya followers ndani ya saa 24 tu kwenye Instagram, tukio lililozua gumzo kubwa kwa mashabiki wa burudani, michezo na lifestyle duniani kote.

Akaunti rasmi ya Instagram ndiyo iliyoongoza kwa kupungua followers baada ya kupoteza zaidi ya milioni 10.9, huku mastaa maarufu wakifuata kwa karibu katika orodha hiyo ya kushangaza.

Nyota wa soka Cristiano Ronaldo ambaye bado anatajwa kuwa mmoja wa watu wenye followers wengi zaidi duniani, amepoteza followers milioni 6.6 ndani ya siku moja. Hasimu wake mkubwa Lionel Messi naye alipoteza milioni 4.8 licha ya kuendelea kuwa na mashabiki wengi duniani.

Katika upande wa muziki na Hollywood, Selena Gomez alipoteza followers milioni 5.4 huku Ariana Grande akishuka followers milioni 5.5 ndani ya muda huo mfupi.

Familia maarufu ya Kardashians nayo haikuachwa nyuma. Kim Kardashian alipoteza followers milioni 5.1, wakati Kylie Jenner akipoteza milioni 5.0 na Khloé Kardashian akishuka followers milioni 3.7.

Muigizaji maarufu Dwayne Johnson maarufu kama “The Rock” naye alipoteza followers milioni 4.8 huku malkia wa muziki Beyoncé akipungua followers milioni 4.4.

Ingawa wengi wamebaki wakishangazwa na takwimu hizo, wataalamu wa mitandao wanaamini huenda Instagram imeendelea na oparesheni ya kufuta akaunti fake, bots na akaunti zisizo hai ili kuboresha mfumo wa matumizi kwa watumiaji wake duniani.

Pamoja na anguko hilo la ghafla, mastaa hao bado wanaendelea kutawala dunia ya burudani na mitandao ya kijamii kwa ushawishi mkubwa, mikataba ya matangazo na jeshi kubwa la mashabiki wanaowafuatilia kila siku.


Hakuna maoni: