Breaking


Ijumaa, 8 Mei 2026

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AWASILI MIKUMI KUZINDUA HOTELI YA MIKUMI WILDLIFE LODGE

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb.), amewasili katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro kwa ajili ya kuzindua Hoteli ya Mikumi Wildlife Lodge pamoja na kufanya ziara ya kikazi mkoani humo.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu ameambatana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba Kabudi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Maliasili na Utalii, Bw. Nkoba Mabula, pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara na taasisi zake.


Uzinduzi wa Hoteli ya Mikumi Wildlife Lodge unatarajiwa kuongeza chachu katika sekta ya utalii kwa kuvutia watalii zaidi kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, hatimaye kuongeza idadi ya watalii na pato la Taifa kwa ujumla

Hakuna maoni: