Jaketi hilo lilikuwa limepambwa kwa alama za kijani zilizokuwa na majina ya wanafunzi 39 pamoja na walimu saba wanaoripotiwa kutekwa katika Jimbo la Oyo, nchini Nigeria. Aidha, nyuma ya jaketi hilo kulikuwa na maandishi yaliyosomeka “Bring Them Home” (Warudisheni Nyumbani), yakihamasisha juhudi za kutafuta na kuwarejesha waliopotea.
Hatua hiyo ya Davido imeibua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, huku wengi wakisifu namna alivyotumia jukwaa kubwa la kimataifa kuwasilisha ujumbe wenye umuhimu wa kijamii.Tukio hilo linaonyesha kuwa mitindo ya mavazi (fashion) inaweza kuwa zaidi ya suala la mwonekano pekee. Mbali na kuongeza mvuto, mavazi yanaweza kutumika kama njia ya kuelimisha jamii, kuhamasisha mabadiliko chanya na kuibua mijadala kuhusu masuala muhimu yanayoathiri watu katika jamii.
Wataalamu wa mawasiliano wanaeleza kuwa matumizi ya sanaa na mitindo ya mavazi katika kuwasilisha ujumbe yanaweza kuongeza uelewa wa umma na kusaidia kuvuta umakini wa watu wengi kuhusu changamoto mbalimbali za kijamii.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni