Ziara hiyo iliyofanyika Juni 4, 2025, imelenga kuwapa madiwani nafasi ya kufahamu kwa undani mifumo ya uendeshaji wa bandari, huduma zinazotolewa, pamoja na maboresho yanayoendelea kufanywa ili kuongeza ufanisi katika usafirishaji na biashara.
Akizungumza wakati wa mapokezi ya wageni hao, Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Abed Gallus Abed, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mkeli Mbossa, alisema TPA inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuboresha huduma za bandari ili kuongeza ushindani na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Kwa upande wao, madiwani wa Manispaa ya Temeke walieleza kuwa ziara hiyo imewapa uelewa mpana kuhusu shughuli za bandari na mchango wake katika kukuza biashara, uwekezaji na ajira kwa wananchi wa Tanzania.
Bandari ya Dar es Salaam ni lango muhimu la biashara kwa Tanzania na nchi jirani, ambapo inaendelea kuboreshwa ili kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye ya usafirishaji wa mizigo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni