Breaking


Jumatano, 24 Juni 2026

MPANGO WA MATTEI NI FURSA KWA TANZANIA. BALOZI MUSSA

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa amefanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Giuseppe Coppola katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam Juni 23, 2026.

Mazungumzo hayo yalijikita katika kupitia utekelezaji wa Mpango wa Mattei nchini Tanzania ambao ni fursa ya kimkakati ya kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Italia.

Kikao hicho kilihusisha wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali za Serikali kwa lengo la kuimarisha uratibu na kuhakikisha mipango ya utekelezaji wa mpango huo inafanyika kwa ufanisi.

Katika kikao  hicho, Balozi Said alieleza kuwa Mpango wa Mattei ni jukwaa muhimu la kuendeleza ushirikiano wa pande mbili na kufanikisha maendeleo yenye tija. Aidha, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi mbalimbali katika kufikia malengo ya mpango huo na kuongeza manufaa yatokanayo na utekelezaji wake.

Kwa upande wake, Mhe.  Balozi Coppola alieleza umuhimu wa kuharakisha utekelezaji wa miradi chini ya Mpango wa Mattei na kuimarisha uratibu kati ya wadau husika ili kuongeza ufanisi na tija katika kufanikisha malengo yaliyokusudiwa. 

Hakuna maoni: