Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano wa NEMC, Martha Kawishe, amesema kuwa mafanikio ya uhifadhi wa mazingira yanategemea ushiriki wa wadau wote.
Amesema changamoto za mazingira, ikiwemo uchafuzi wa mazingira, utupaji holela wa taka na shughuli zinazoweza kuharibu ikolojia, zinahitaji juhudi za pamoja ili kudhibitiwa kwa ufanisi.
Kawishe amesisitiza umuhimu wa wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka husika wanapobaini vitendo au shughuli zinazohatarisha mazingira katika maeneo yao.Amesema ushirikiano huo utasaidia mamlaka kuchukua hatua kwa wakati na kuzuia madhara yanayoweza kuathiri afya za wananchi, uchumi na mazingira kwa ujumla.
Aidha, NEMC itaendelea kutoa elimu kwa umma na kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika usimamizi na uhifadhi wa mazingira nchini.
Kutokana na hali hiyo, amewashauri wananchi, wafanyabiashara na wawekezaji kuwa makini wanapokutana na watu wanaodai kuwa maafisa wa NEMC.
Amesema kabla ya kuruhusu ukaguzi wowote, ni muhimu kuomba kuonyeshwa kitambulisho cha kazi, kitambulisho maalumu cha ukaguzi wa mazingira pamoja na nyaraka rasmi zinazompa mhusika mamlaka ya kufanya ukaguzi huo.
NEMC imeeleza kuwa tahadhari hiyo itasaidia kudhibiti vitendo vya udanganyifu na kulinda maslahi ya wananchi pamoja na wawekezaji nchini.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni