Breaking


Jumatano, 10 Juni 2026

RAIS WA SINGAPORE AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MWINYI ZANZIBAR



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amempokea Rais wa Jamhuri ya Singapore, Tharman Shanmugaratnam, aliyewasili Zanzibar pamoja na ujumbe wake rasmi kwa ziara ya kikazi.

Rais Tharman aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akitokea Dar es Salaam, ambapo alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, urafiki na ushirikiano wa maendeleo kati ya Tanzania na Singapore katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.



Baada ya mapokezi hayo, viongozi hao wawili walifanya mazungumzo rasmi Ikulu Zanzibar, yakijikita katika masuala ya ushirikiano na fursa za maendeleo zinazoweza kuzinufaisha pande zote mbili.


Rais Tharman yupo nchini kwa ziara ya siku tatu na anatarajiwa kurejea Dar es Salaam baadaye leo kabla ya kuhitimisha ziara yake na kuondoka nchini usiku wa leo.

Hakuna maoni: