Serikali imeeleza kuwa sehemu kubwa ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 ya Shilingi trilioni 62.3 itagharamiwa na mapato ya ndani, hatua inayoendelea kuimarisha uwezo wa nchi kujitegemea katika kufadhili maendeleo yake.
Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar,amesema mapato ya ndani yanatarajiwa kufikia Shilingi trilioni 46.8 katika mwaka ujao wa fedha na kuchangia kwa kiwango kikubwa utekelezaji wa bajeti hiyo.
Amesema mafanikio hayo yanatokana na kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani pamoja na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali kuimarisha usimamizi wa rasilimali za umma.
Kwa mujibu wa Waziri huyo, fedha zitakazopatikana zitawezesha Serikali kuendelea na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo Reli ya Kisasa ya SGR, miundombinu ya barabara, miradi ya maji, nishati na maendeleo ya rasilimali watu.
Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha usimamizi wa matumizi ya fedha za umma ili kuhakikisha kila shilingi inayokusanywa inatumika kwa tija na kuwanufaisha wananchi.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni