Na Beda Msimbe,TBN, Moscow
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi- (RUDN University) huku akiitoa shahada hiyo kwa Watanzania.
Shahada hiyo ilitolewa na Mkuu wa Chuo hicho Profesa Oleg Yastrebov kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo Moscow nchini Urusi, tarehe 04 Juni,2026.
Rais Mhe. Dk Samia ametunukiwa Shahada hiyo ya Uzamivu kutokana na mchango wake katika Mageuzi ya sekta ya Elimu, juhudi zake za kuimarisha Diplomasia ya Tanzania,
pamoja na mchango wake katika kuimarisha hadhi ya Tanzania Kimataifa ikiwemo kupitia sekta ya Utalii,
Akizungumza baada ya kupewa shahada hiyo Rais Samia alisema kwamba heshima aliyopewa si ya mafanikio yake binafsi bali ni utambuzi wa juhudi na matarajio ya watanzania wote.
Alisema shahada hiyo ni ishara ya utambuzi wa dhamira ya pamoja ya Watanzania wote katika kuleta maendeleo,ushirikiano na ustawi wa binadamu.
“Nilipokea kwa furaha habari za kutunukiwa heshima hii,lakini mara moja nikatambua kwamba si yangu peke yangu. Ni heshima inayoitambua dhamira yetu ya pamoja ya maendeleo, ushirikiano na maendeleo ya binadamu” alisema Dk Samia.
Hii ni shahada yake ya nane kutolewa kwa Rais Samia .
Aidha alisema shahada hiyo aliyopewa leo ni ishara ya urafiki wa muda mrefu kati ya Tanzania na Urusi ikiwa ni uthibitisho wa nafasi muhimu ya elimu katika kuunganisha mataifa.
Aidha alisema heshima hiyo inaakisi uhusiano wa kudumu kati ya nchi za Tanzania na Urusi ambazo zimeendelea kushirikiana katika sekta mbalimbali hususani elimu kwa miongo kadhaa sasa.
Katika hotuba yake ambayo viongozi wa watanzania waliopo Urusi na vyuo vya Urusi walisema ni iluiyiojaa mamlaka makubwa, Rais Samia alisema kwa miaka mingi watanzania walikuwa wanapata elimu inayochangia maendeleo ya Tanzania katika Nyanja mbalimbali jambo ambalo pia limeimarisha mahusiano ya watu wa pande zote mbili,
“Mama amezungumza nchi yetuj ina sifa sana. Tena sifa njema kwa kupata mwaliko wa Rais Vladmir Putin kuja hapoa ni kutambulika kwa Tanzania ni ishara njema na hotuba ya mama imeakisi matarajio” alisema Jefrey Mashauri Mwenyekiti wa wanafunzi wa Tanzania shirikishoi la Urusi (TASCARU).
Naye Mwenyekit wa watanznaia wanaoishi Urusi Pascal Gura alisema watanzania 300 wanaosihi hapo wameona fahari kubwa kukutana na kumsikiliza Rais Samia akionesha ni kwa namna gani kama Taifa Tanzania linaendelea kuwika.
Rais Samia katika hotuba yake alionesha jinsi Tanzania inavyoweza kufanikisha mambo wanaposaidiana na kushirikiana kwa maendeleo ya taifa.
Pia alikumbusha vijana kujipatia elimu huku wakizingatia kauli ya baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere ambaye alifundisha kwamba maendeleo lazima daima yaweke mwanadamu katikati ya kila jambo.
Aidha alitaka vijana kuangalia taifa lao na kwamba dokumentari iliyooneshwa kabla ya kutunukiwa shahada kuhusu maendeleo ya Tanzania inawaonesha dhamira ya watanzania na ni muhumu kwao watambue umuhimu wao kwa taifa huku huku wakiyaakisi maneno ya baba wa taifa katika utumishi wao.
Tangu kuanzishwa kwa chuo hicho miaka ya 1960 watanzania 1,100 wamepata utaalamu mbalimbali kupitia hucho hicho.Idadi hiyo ni kati ya wanafunzi 5000 ambao wamepata taaluma zao nchini Urusi katika Nyanja mbalimbali ikiwamo udaktari uhandisi na wataalamu wa sayansi.
Rais katika hotuba yake pia alizungumzia makubaliano kadhaa yaliyotiwa saini yenye lengo la kuleta ushirikiano wa aina yake katika utafiti na elimu na ufundishaji.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni