Kwa mujibu wa taarifa zinazozunguka kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 na raia wa Congo Brazzaville amefikia makubaliano binafsi na Yanga, huku akitarajiwa kuwasili Tanzania kwa ajili ya kukamilisha taratibu za mwisho za usajili na kusaini mkataba wa miaka miwili.
Fred Ngoma anatajwa kuwa mmoja wa viungo waliotoa kiwango kizuri msimu uliopita, hususan katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, jambo lililovutia klabu mbalimbali, ikiwemo Yanga.
Hata hivyo, hadi wakati wa kuchapisha taarifa hii, Yanga SC haijatoa tangazo rasmi la kuthibitisha usajili wa mchezaji huyo. Mashabiki wa klabu hiyo wanaendelea kusubiri taarifa rasmi kutoka uongozi wa Yanga kuhusu hatma ya dili hilo.
Endapo usajili huo utakamilika, Fred Ngoma anatarajiwa kuongeza nguvu katika eneo la kiungo huku Yanga ikiendelea kujiimarisha kuelekea msimu mpya wa mashindano.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni