Afisa Mnadhimu wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Rajabu Shemndolwa, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillus Wambura, amewatunuku vyeti vya sifa na zawadi Askari 45 wa Makao Makuu ya Jeshi hilo waliofanya vizuri zaidi kiutendaji katika kipindi cha mwaka 2025/2026, katika hafla iliyofanyika leo, Agosti 28, 2026 Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dodoma.
Akizungumza katika hafla hiyo, ACP Shemndolwa amewataka askari hao kutumia pongezi na zawadi walizotunukiwa kama chachu ya kuendelea kufanya vizuri zaidi katika kutekeleza majukumu yao.
Amesisitiza kuwa huduma wanazozitoa kwa jamii zinapaswa kuzingatia misingi ya nidhamu, haki, weledi na uadilifu.
Utoaji wa vyeti vya sifa na zawadi ni sehemu ya utaratibu endelevu wa Jeshi la Polisi Tanzania wa kutambua na kuthamini mchango wa watumishi wake wanaofanya vizuri zaidi katika utekelezaji wa majukumu yao.







Hakuna maoni:
Chapisha Maoni