Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali kutoka kwa waandishi wanaofuatilia soko la usajili, pande zote mbili zimepiga hatua kubwa katika mazungumzo baada ya kikao kilichofanyika Jumatano. Inaelezwa kuwa Vinicius Jr pamoja na wawakilishi wake wametoa mwanga wa awali wa kukubali masharti ya mkataba huo, huku maelezo ya mwisho yakifanyiwa kazi kabla ya makubaliano rasmi kufikiwa.
Endapo kila kitu kitaenda kama kinavyotarajiwa, nyota huyo wa kimataifa wa Brazil atasaini mkataba mpya katika kipindi kifupi kijacho, jambo litakaloimarisha nafasi yake kama mmoja wa wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha Real Madrid.Wakati huo huo, taarifa hizo pia zinadai kuwa kocha José Mourinho amekuwa akisisitiza umuhimu wa Vinicius Jr kuendelea kubaki katika klabu hiyo, ingawa hakuna tamko rasmi lililotolewa kuhusu madai hayo.
Hadi sasa, Real Madrid na Vinicius Jr hawajatoa taarifa rasmi kuhusu kukamilika kwa mkataba huo, hivyo mashabiki wanasubiri uthibitisho kutoka kwa klabu hiyo kuhusu mustakabali wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni