Breaking


Jumatatu, 10 Agosti 2026

DKT. SAMIZI AONGOZA VIKAO VYA WIZARA YA AFYA, ASISITIZA TAARIFA SAHIHI NA ZENYE USHAHIDI



 Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi, leo Agosti 10, 2026 ameongoza vikao na wataalamu kutoka Wizara ya Afya kwa lengo la kupitia na kujadili taarifa za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, pamoja na masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara katika sekta ya afya.

Dkt. Samizi ameendesha vikao hivyo kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, ambapo amesisitiza umuhimu wa wataalamu wa Wizara kuhakikisha taarifa zinazowasilishwa kwa Kamati zinakuwa sahihi, zenye takwimu na ushahidi unaoeleweka, pamoja na kuakisi utekelezaji halisi wa shughuli za Wizara.

Aidha, katika vikao hivyo, Naibu Waziri amepokea na kujadili maelezo kutoka kwa wataalamu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa mipango na mikakati ya Serikali katika kuimarisha huduma za afya na kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika sekta hiyo.

Dkt. Samizi ameelekeza wataalamu kuhakikisha hoja na mapendekezo yanayotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI yanapatiwa majibu na hatua stahiki kwa kuzingatia miongozo, sera na mipango ya Serikali.

Hakuna maoni: