Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde ametoa rai kwa Wananchi Nchini kuchukua tahadhari na kuhifadhi chakula walichovuna mwaka huu, kufuatia utabiri wa Mamlaka za Hali ya Hewa Nchini na Kimataifa kuhusu uwezekano wa kutokea kwa mvua za El Niño.
Silinde ameyasema hayo hii leo Agosti 26, 2026 Bungeni Jijini Dodoma katika Bunge la 13, Mkutano wa nne, Kikao cha Kwanza wakati akijibu swali la Nyongeza la Mounge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Nancy Hassan Nyalusi ambapo aliuliza ni lini Serikali itaanza kununua mahindi ya Wakulima?
Akijibu Swali hilo Silinde amesema "Nitoe rai kwa Wananchi kuwa tumesikia taarifa zimetolewa na Mamlaka za Hali ya Hewa Nchini na Duniani kuhusu uwepo wa utabiri wa mvua za EI Niño kwa mwaka huu maana yake kama kutakuwa na El Niño, hivyo kutakuwa na changamoto katika uzalishaji na kama kutakuwa na changamoto katika uzalishaji maana yake tunaweza kuwa na hatari kubwa ya uwepo wa njaa katika mwaka unaofuatia, hivyo tutunze chakula,".

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni