Breaking


Jumatano, 19 Agosti 2026

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YAKUTANA NA TCAA NA TAA KUJADILI MWENENDO WA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA

 

Kamati ya  Bunge ya Bajeti imekutana na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi  kwa lengo la Kupokea na kujadili taarifa kuhusu mwenendo wa Sekta ya Usafiri wa anga nchini, mafanikio na changamoto za kikodi.




Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Mh. Mashimba Ndaki imepokea ufafanuzi na majibu kutoka kwa taasisi hizo na Pamoja na Wizara ya Uchukuzi ikiongozwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mh. David Kihenzile katika kutoa maelekezo ya kuhakikisha yote yaliyojadiliwa na kuafikiwa katika kikao hicho yanatekelezwa kwa wakati. Kikao hicho kimefanyika Agosti 18, 2026 jijini Dodoma.

Hakuna maoni: