Kwa mujibu wa taarifa zinazosambaa, Owori alishambuliwa na watu wasiojulikana alipokuwa akirejea nyumbani usiku wa kuamkia leo. Baada ya tukio hilo alipelekwa hospitalini kwa matibabu, lakini baadaye alifariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata.
Owori alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa wamejumuishwa katika kikosi cha awali cha timu ya taifa ya Uganda kinachojiandaa na mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yatakayofanyika nchini Morocco.
Kifo chake ni pigo kubwa kwa SC Villa, timu ya taifa ya Uganda na mashabiki wa soka barani Afrika. Viongozi wa klabu, wadau wa michezo na mashabiki wameendelea kutuma salamu za pole kwa familia ya marehemu pamoja na wote walioguswa na msiba huo.
Madelemo News inaungana na familia, marafiki, SC Villa na jamii yote ya soka nchini Uganda kutoa pole kufuatia msiba huu. Taarifa zaidi kuhusu tukio hilo zitatolewa kadri zitakavyopatikana kutoka kwa mamlaka husika.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni