Breaking


Jumanne, 18 Agosti 2026

TMA YATOA TAHADHARI YA EL NINO KUATHIRI MVUA ZA VULI



Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania-TMA, imetoa tahadhari ya kuwepo kwa mvua za El Nino zitakazoathiri msimu wa mvua za Vuli unaotarajiwa kuanza mwezi Oktoba 2026 na kuendelea hadi mwezi Januari mwakani.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang’a, amesema msimu wa mvua za Vuli 2026 unatarajiwa kuathiriwa kwa kiwango kikubwa na hali ya El Nino yenye nguvu kubwa, huku mvua za juu ya wastani hadi wastani zikitarajiwa katika maeneo mengi.

Mvua hizo zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya Septemba hadi wiki ya kwanza ya Oktoba 2026 katika maeneo ya Ukanda wa Ziwa Victoria na baadaye kusambaa katika maeneo mengine mwezi Oktoba.

Mvua za juu ya wastani hadi wastani zinatarajiwa katika Kanda ya Ziwa Victoria, ikijumuisha Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara, pamoja na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma.

Aidha, amesisitiza wito wa tahadhari kwa wadau wa mifugo na uvuvi, utalii na wanyamapori, nishati na madini, sekta ya afya, Serikali za Mitaa, ujenzi, sekta binafsi pamoja na Menejimenti za Maafa za wilaya, mikoa na kitaifa ili kuendelea kuratibu mipango ya kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.

Nao, baadhi ya wavuvi katika Soko la Kimataifa la Feri jijini dar es salaam, akiwemo Musa Rashid na Jackson Mbuya, wameeleza namna mwelekeo huo wa mvua unavyoweza kuwa na athari katika shughuli zao za uvuvi.

Hakuna maoni: