Breaking


Jumamosi, 22 Agosti 2026

VIJIJI NA VITONGOJI VYOTE TANZANIA BARA KUWA NA UMEME KABLA YA MWAKA 2030

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa hatua kubwa iliyofikiwa katika kusambaza umeme nchini, huku akiwataka kuongeza kasi ya kufikisha huduma hiyo kwenye maeneo yaliyosalia.

Rais Samia amesema Serikali imeendelea kupanua wigo wa upatikanaji wa umeme kwa wananchi kote nchini, ambapo hadi sasa vijiji vyote 12,318 na takribani asilimia 62.4 ya vitongoji Tanzania Bara vimefikiwa na huduma ya umeme.

Amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Tanzania nzima inapata umeme ifikapo mwaka 2030, akieleza matumaini kuwa lengo hilo linaweza kufikiwa kabla ya muda uliopangwa. “Dhamira yetu ni kuhakikisha nchi yote inapata umeme ifikapo mwaka 2030 na nadhani tutafikisha lengo hili kabla ya 2030,” amesema.

Aidha, Rais Samia amewapongeza wadau wa maendeleo, hususan Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Benki ya Dunia, kwa mchango wao katika kuwezesha juhudi za Serikali za kufikisha umeme vijijini na kuongeza upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi.


Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, Agosti 22, 2026, wakati akizungumza na wananchi Mkoani Pwani mara baada ya kuzindua Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Megawati 2,115 wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere.

Hakuna maoni: