Waziri wa Afya Mohamed Mchengerwa akiwasili katika Mkutano wa Nne wa Kamati ya Uongozi ya Ukanda wa Afrika wa Mawaziri wa Afya (ReSCO) unafanyika leo tarehe 18 - 19 Agosti 2026 Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mchengerwa ambaye ni Makamu Mwenyekiti na mwenyeji wa Mawaziri kutoka nchi 14 Barani Afrika ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe kwenye mkutano huo wa kitaalam Kanda ya Afrika unaobeba agenda ya Afya ya Uzazi mama, mtoto na vijana sanjari na agenda ya kukabiliana na magonjwa ya Mlipuko katika nchi za Afrika.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni