Breaking


Jumatano, 9 Septemba 2026

DIAMOND PLATNUMZ AMFARIJI RAIS SAMIA KUFUATIA KIFO CHA MUMEWE

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, amemtembelea na kumpa pole Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba wa mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.


Diamond Platnumz amefika nyumbani kwa Rais Samia huko
Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, leo Septemba 9, 2026, ambapo ametoa salamu za pole na faraja kufuatia msiba huo.


Maalim Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Septemba 7, 2026, akiwa katika
Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar.

Ziara hiyo ni sehemu ya hatua za kuwafariji wafiwa na ndugu wa marehemu katika kipindi hiki cha maombolezo.


Taarifa na picha kutoka katika tukio hilo zimeendelea kusambaa kupitia mitandao ya kijamii, zikionyesha Diamond Platnumz akimpa pole Rais Samia kufuatia msiba huo.

Madelemo News inaendelea kuwafikishia wasomaji taarifa mbalimbali kuhusu matukio yanayoendelea nchini.


Hakuna maoni: