Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Saada Salum Mkuya, amesema hayo katika Baraza la Wawakilishi Chukwani, Visiwani Zanzibar, alipokuwa akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayubu.
Waziri Mkuya amesema kwa sasa mahitaji ya Drip Zanzibar yanafikia chupa 452,338 kwa mwaka.
Aidha, amebainisha kuwa kwa kuzingatia mahitaji hayo pamoja na matarajio ya kuongezeka kwa matumizi, Wizara kupitia Wakala wa Bohari Kuu ya Dawa imepanga kupata mtambo wenye uwezo wa kuzalisha kati ya chupa 500,000 hadi milioni mbili kwa mwaka.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni